Wednesday, October 5, 2016

YOTE UNAYOTAKIWA KUJUA KUHUSU GOOGLE PIXEL

Habari na karibu ndani ya equatortech kwa ajili ya taarifa za teknologia kwa lugha ya  kiswahili.
Leo napenda kuwaelezea simu mpya kutoka google inayoitwa pixel 
Google pixel inauwezo wa kutumika kiraisi kwa ajili ya manufaa ya mteja
pixel ni nzuri lkn inayoifanya iwe hai ni mungano wa vifaa vya ndani na njee vya simu hiyo.
Ningependa kuwaeleza vitu 5 vizuri ndani ya simu hii

1)Google msaidizi 

 Pixel ndo simu ya kwanza kuwa na google msaidizi.
 ukiwa na  Google msaidizi (GOOGLE ASISTANT) ni vizuri sana kwa kuboyeza kitufe cha nyumbani(home buton) na kunena unachokitaka  mfano unaeza sema "play wimbo mpya wa diamond" ama ukiambia tafazali mtumie juma ujumbe na umwambie "NAKUJA" na yenyewe ina fanya kazi ama unaeza kuiambia kwamba "mwambie tukutane wap" na yenyewe ikajua ni wapi na kadhallika
pia inaeza kukusaidia vitu vikubwa na vidogo kama unavopenda kama kuseti alarm ya mda mwafaka kwa maneno tu lakini kwa lugha ya kingereza.

2)Picha

Camera ya simu hii imetengenezwa kutoka kampuni ya DXO MARK na simu hii imepewa alama ya 89% na ambayo ni alama ya simu za smart ya juuu kuliko zote duniani.Google pixel imepewa camera yenye Smartburst ambayo ni kusaidia kupiga picha ya hali ya juu. pia imepewauwezo wa kupiga na kuhifazi picha kwa mda mfupi na kukufanya wewe  kuweza kupiga picha nyingi kwa mda mfupi.Na application ya camera inauwezo wa kufunguka upesi ili usichelewe kuchukua picha kwajili ya mwendo mdogo wa camera yako.Na kitu kingine ambacho ni kizuri kuhusu simu ni CAMERA STABILIZATION kwamba kamera inauwezo wa kuchukua matukio kwa usanifu hata kama wewe hauja tulia hii itakusaidia wewe mtumiaji kurekodi matukio vizuri hata kama unakimbia huku una rekodi.Utakapo nunua kamera hii utakapo nunua simu hii utapewa ofa ya kuhifazi picha na video ndani ya google cloud bila kikomo ili usiishiwe na memory ya kwa jili ya vitu vyako.
  

3 mawasiliano mazuri

 Haijalishi maafiki na ndugu zako wapo ndani ya ios ama android kwa kutumia google duo utaweza kuwasiliana nao kiurahisi zaidi. pia kwa kutumia google duo simu hii utaweza kuangalia mtu anafanya nini na ni nani anaye kupigia kabla hata ya kupokea simu hiyo. kwa kuhakikisha unaeza kuwasiliana kwa ubora google pixel imekuja na betri mahususi simu hiii utaeza kutumia masaaa 7 kwa kuichaji ndani ya dakika 15. Pia itaeza kuapdate yenyewe bila kukusumbua.
 Pixel inakuja katika saiz mbili ya inchi 5 na inchi 5.5 kila kitu vinfanana kwenye simu zote mbili utofauti ni size ya kioo tu inakuja kwa rangi tatu kuu NYEUSI,NYEUPE NA BLUE.

***HABARI HIZI ZINALETWA KWENU NA EQUATOR TECHNOLOGY KWA AJILI KUKUPA TARIFA ZA KISWAHILI*****